Habari za Kaunti

Watu sita waaga dunia, watano wapofuka baada ya kubugia pombe ya sumu

February 6th, 2024 1 min read

NA MWANGI MUIRURI

WATU sita wameaga dunia huku wengine watano wakipofuka macho kwa muda katika Kaunti ya Kirinyaga baada ya kubugia pombe ya sumu.

Kwa mujibu wa Naibu Kamishna wa Mwea Mashariki Teresiah Mwangi, mkasa huo umetokea katika kijiji cha Kangai katika baa iliyotambuliwa kama California.

Afisa huyo alitaja kisa hicho kuwa cha kufedhehesha.

Alijitetea kwamba maafisa wake wamekuwa wakijaribu kuzuia mkasa huo kupitia kuvamia baa hiyo.

“Lakini juhudi zetu zimekuwa zikiambulia patupu kupitia ilani za mahakama za kutuzima kumtia mbaroni mmiliki na kufunga baa yake,” akasema Bi Mwangi.