Habari Mseto

Watu wanne wafariki, 12 wajeruhiwa katika ajali iliyohusisha lori na matatu Man Eaters

November 20th, 2019 1 min read

Na LUCY MKANYIKA

WATU wanne wamefariki huku 12 wakijeruhiwa baada ya lori na matatu kugongana dafrao eneo la Man Eaters katika barabara kuu ya Nairobi-Mombasa.

Kamanda wa polisi kaunti ndogo ya Voi Bernstein Shari amesema matatu iliyokuwa ikielekea Mombasa ilikuwa na inayapita magari mengine katika eneo la barabara palipo na kona wakati ajali hiyo ilitokea.

Miongoni mwa majeruhi 12 ni madereva wa magari hayo mawili na walipelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Moi mjini Voi, Kaunti ya Taita Taveta.

Oktoba 26, 2019, watu wanne walifariki magari mawili madogo yalipogongana dafrao karibu na Emali barabara kuu ya Nairobi-Mombasa.