Habari

Watu wanne wafariki Kitui baada ya gari lao kusombwa na maji ya mto uliofurika

October 17th, 2019 1 min read

Na KITAVI MUTUA

WATU wanne wamefariki baada ya gari lao kusombwa na maji ya mto uliofurika wakati wakivuka eneo la Matinyani, Kaunti ya Kitui, amethibitisha OCPD John Sawe.

Kufikia sasa miili ya watatu imeshaopolewa kutoka mtoni , lakini wa nne umenasa kwenye gari ambalo limepondeka.

Wahanga ambao tayari wametambulika ni kaka wawili pamoja na mhandisi; wote ambao wamekuwa wakiifanyia kazi kampuni ya teknolojia ya Trade Telecoms.

Waokoaji tayari wanajaribu kuondoa mwili ulionasa kwenye gari.

OCPD Sawe amesema watu wawili walinusurika.

“Wawili waliogelea na wakafanikiwa kutoka na kwa sasa wamepelekwa hospitalini ili wakatibiwe,” amesema Sawe.