Habari Mseto

Wauguzi Embu wasitisha mgomo

September 28th, 2020 1 min read

NA GEORGE MUNENE

Maafisa wa Afya wa Kaunti ya Embu Jumapili walikumbali kusitisha mgomo waliokuwa wakiendeleza na kurudi kazini Jumatatu.

Hii inajiri baada ya kaunti  hiyo kuamua kusikiza malalamishi yao na kutia sahihi. Makubaliano hayo yalifikiwa baada ya mkutano kati ya Afisa wa Afya wa Kaunti pamoja wa mwenzake wa Fedha John Njagi.

Mwenyekiti wa Muungano wa Wauguzi Joseph Ngwasi alisema wafanyakazi hao walikuwa na sababu ya kutabasamu kwani serikali ilikubali kusikiza malalamishi yao.

“Tumeridhishwa na hatua zilizochukuliwa na serikali na tutaanza kuwahudumia wagonjwa,” alisema Bw Ngwasi.

Wafanyakazi hao walifanya mgomo baada ya kuchelewesha kwa mshahara na kutolipwa kwa marupurupu ya corona.

Shughuli zote za afya kwenye hospitali ya rufaa ya Embu zilikatizwa na mgomo huo.

Wauguzi hao hao pia walimlaumu gavana Martin Wambora kwa kukosa kutuma pesa.

TAFSIRI NA FAUSTINE NGILA