Habari Mseto

Wauzaji Kongowea walia kutatizwa na genge

April 4th, 2019 1 min read

Na Anthony Kitimo

WAFANYABIASHARA kaunti ya Mombasa wamelalamikia kuwepo kwa kundi la watu wanaowazuia kufanya biashara ndani ya soko la Kongowea.

Mmoja wa wafanyabiashara hao, Bw Cosmas Munene,ambaye pia ni mkulima ambaye amewahi kupata hasara kutokana na genge hilo, alisema imembidi atafute soko mbadala.

“Mara ya kwanza nilikuwa na lori la tomato na licha ya kulipa ada ya soko, walinizuia kuingiza mali yangu sokoni kwa madai sijasajiliwa katika soko hilo,” alisema Bw Munene.

Afisa wa Chama cha Wafanyabiashara katika soko hilo, Bw Peter Nyaga, alisema visa kadha vimeripotiwa lakini hakuna hatua zimechukuliwa kwani. watu hao ni kama wanashirikiana na mabwenyenye mjini Mombasa.

Juhudi za Taifa Leo kupata taarifa kamili kutoka kwa afisa wa biashara kaunti ya Mombasa Abdulwahab Mubarak ziligonga mwamba kwani alihitaji muda kutupa taarifa kamili kuhusu kundi hilo licha ya kumtumia maswali hayo.