Wauzaji pombe taabani kwa kukwepa ushuru wa 4.5m

Wauzaji pombe taabani kwa kukwepa ushuru wa 4.5m

Na RICHARD MUNGUTI

WAUZAJI wa pombe walishtakiwa Jumatatu kwa kukwepa kulipa ushuru wa sh4.5 milioni.

Margaret Waithera Kariuki, Samuel Kihara Wakabi na Peter Mwangi Gichuhi walishtakiwa mbele ya hakimu mwandamizi Bw Kennedy Cheruiyot.

Walikanusha mashtaka ya kuhifadhi pombe ambayo haikuwa imelipiwa ushuru.

Maafisa wa Mamlaka ya Ushuru nchini, KRA waliwapata washukiwa hao katika kituo chao cha biashara cha Barak Mowlem Business Centre.

Walikuwa na katoni 170 za pombe kali ijulikanayo kama  Turkeys Pioneer. Pia walikuwa na Vodka Blue katoni 198.

Mahakama ilifahamishwa kuwa washukiwa hao walipatikana na stempu feki 24,000 za kuweka kwenye pombe hiyo kuthibitisha zimelipiwa ushuru.

You can share this post!

Wachimba mawe walia kuteswa

Mhispania kizimbani kwa kumlaghai Mwitaliano Sh14m

adminleo