Wawaniaji Azimio wakimbilia Raila

Wawaniaji Azimio wakimbilia Raila

NA KENYA NEWS AGENCY

WAWANIAJI wanaoegemea Azimio La Umoja One Kenya katika Kaunti ya Kisii, wamemsihi mgombea urais wa muungano huo, Raila Odinga, kuingilia kati na kusuluhisha tofauti zinazoshuhudiwa baina yao.

Katika siku za hivi majuzi, Kaunti hiyo imeshuhudia visa vya ghasia, wagombeaji kuhangaishwa na uharibifu wa vifaa vya kampeni vya wawaniaji, jambo ambalo limesababisha muungano wa Azimio kulaumiana kuhusu matukio hayo.

Akihutubia wanahabari katika eneobunge la Bobasi, Mbunge wa Kitutu Chache Kusini, Richard Onyonka alisema Bw Odinga anapaswa kuwaunganisha wagombeaji wa Azimio.

You can share this post!

Gachagua aahidi kupiga marufuku mchele wa nje

Chebukati anaficha nini?

T L