Habari Mseto

Wawili wafariki kwenye ajali Pwani

August 24th, 2020 1 min read

NA Maureen Ongala

Watu waliwili walifariki  na wengine 18 wakaumia kwenye  ajali mbili tofauti zilizotokea kwenye barabara ya Mombasa kuelekea Kilifi eneo la Shauri Moyo Jumatatu.

Kamanda wa polisi Kaunti Ndogo ya Kilifi Kusini Joseph Wako alisema kwamba ajali ya kwanza ilikuwa kati ya Lori na gari ndogo huku ajali ya pili ikihusisha gari mbili ndogo na matatu.

“Kwenye ajali ya kwanza dereva wa lori alikuwa akipita bila kujali alipogangana na Land cruiser .Kwenye ajali ya pili dereva wa Subaru aligongana na BMW na matatu iliyokuwa ikitoka Kilifi,” alisema Bw Wako.

Aliyeshuudia ajali hiyo Suleiman Charo kutoka Takaungu alisema kwamba alikuwa ameabiri matatu kuelekea mahala anapofanya kazi Vipingo ajali hio ilipotokea muda mchache.

Bw Charo alisema kwamba kulikuwa na abiria  saba kwenye matatu hiyo.

“Dereva wa gari hiyo ndogo kutoka Mombasa alikuwa anaendesha gari kwa kasi na kupita gari ingine kupitia mwelekeo mmoja .Dereva wetu alihepa kutoka kwa barabara huku gari hio ndogo ikigongana kichwa kwa kichwa na matatu ililiyokuwa ikieleka Mombasa .Tuko bahati sana tulinusurika,”alisema.

TAFSIRI: FAUSTINE NGILA