Habari Mseto

Wawili waliomuua mteja wa M-Pesa watafutwa

August 7th, 2020 1 min read

NA MOHAMED AHMED

Polisi wanatafuta wanaume wawili waliomuua mteja mmoja wa M-Pesa na kuiba hela kiasi kisichojulikana kwenye mtaa mpana wa Moi, Mombasa.

Ripoti ya polisi inaonyesha kwamba Winnie Kerubo alipigwa risasi ya kifuani Ijumaa saa mbili na nusu asubuhi.

Kerubo ambaye alifanya kazi na kampuni ya Shash alikuwa akipeleka pesa benki.

Alifariki alipokuwa akikimbizwa hospitali ya mafunzo ya Coast General.

Wezi hao walihepa kwa pikipiki ,njia ambayo imekua ikitumiwa na wezi kutekeleza uhalifu.

Mkuu wa DCI Mombasa Antony Muriithi alisema kwamba walihepa na kiasi cha pesa ambacho hakijulikani.