Habari Mseto

Wawili wapatikana wameuawa Rongai

July 1st, 2020 1 min read

PHYLLIS MUSASIA NA FAUSTINE NGILA

Polisi wanachunguza kisa kimoja ambapo watu wawili walipatikana wamefariki kwenye eneo la ujenzi la Olive Inn Kiamunyi kaunti ndogo ya Rongai.

Chifu wa Kiamunyi Wilson Maraga alisema kwamba wafanyakazi wa eneo hilo la ujenzi walipashwa habari hiyo baada ya kufika kazini saa mbili asubuhi Alhamisi.

“Haijajulikana wawili hao waliingia kwa eneo la ujenzi aje na kiini cha kuingia huko na waliowaua ni kina nani, uchunguzi bado unaendelea,” alisema Bw Maraga.

Alisema mwanume aliyekuwao akilinda eneo hilo yuko kituo cha polisi na atasaidia maafisa wa upelelezi kufanya uchunguzi.

Wakazi walisema kwamba wawili hao walikuwa  makanga na wamekuwa wakifanya kazi kwenye kituo cha magari cha Inn.

Kamanda wa polisi wa kaunti ndogo ya Rongai Richard Rotich alisema kwamba walikuwa na wamekatwa na nguo zao zilikuwa zimelowa damu.

Miili yao ilipelekwa kwenye chumba cha kuhifadhi maiti.