Habari Mseto

Wawili wapigwa risasi kwenye maandamano Garissa

July 27th, 2020 1 min read

FARHIYA HUSSEIN na FAUSTINE NGILA

Watu wawili walipigwa risasi kufuatia maandamano yaliotokea kwenye soko la mifugo mjini Garissa.

Kamishena wa kaunti Meru Mwangi alithibitishwa kisa hicho lakini alikuwa bado hajapokea ripoti kamili.

Mashahidi walisema kwamba tukio hilo lilitokea polisi walipokuwa wakiwatafuta watu wawili waliokisiwa kuwa magaidi..

“Walipowapata kwenye gari walikataa kukamatwa huhio ikaelekea kelele kutoka kwa wakazi wakipigia kelele na kupigana na polisi hio ikaeleka na maandamano ,”alisema Ali Abdi mwanabiashara.

Mfanya biashara mwingine ,mariam Kheiry, alisema kwamba wawili hao walikimbia kuelekera kwa hoteli lakini polisi wakawafuata.

“Tulisikia risasi kwenye hoteli .Tulikuta polisi wamewapiga risasi watu wawili waliokuwa kwenye hoteli hio baada ya kuwakosa washukiwa hao,”alisema.

Kufwatia risasi hizo viongozi wa eneo hilo waliomba kupitia mitandao ya kijamii hatua ichukuliwe huku wakiwalaumu poilisi kwa kutumia nguvu kupita kiasi.

“Ninakemea mauaji ya wakenya hao waliwili wasiokuwa na hatia kwenye soko ya mifugo Garissa.Wauaji hao lazima washtakiwe ,”alisema Gavana Ali Korane.

Mwakilishi wa wanawake wa kaunti hio ya Garisa alimuomba Inspeka Generali wa polisi Hilary Mutyambai kuingililia kati.