Habari Mseto

Wawili washtakiwa kuiba Sh5 milioni

June 22nd, 2018 1 min read

Na RICHARD MUNGUTI

WAFANYAKAZI wawili walishtakiwa kwa wizi wa Sh5 milioni Ijumaa. 

Mabw Jacob Kirimi Nkando na James Kyalo Kiema walikanu shtaka la kuiba pesa hizo kutoka kwa kampuni ya Erdemann kati ya Januari 24, 2017 na Machi 19, 2018.

Wakiomba waachiliwe kwa dhamana Bw Kiema ndiye anayehudumia familia yake.

“Mke wangu alijifungua hivi majuzi. Mtoto yuko na umri wa miezi miwili na hafanyi kazi,” alisema Kiema.

Bw Nkando alisema hana mapato ya juu na kuomba aachiliwe kwa kiwango kisicho juu cha dhamana.

Waliachiliwa kwa dhamana ya Sh300,000 pesa tasilimu. Kesi itatajwa baada ya wiki mbili.