Habari za Kitaifa

Wawili wathibitishwa kufariki, mamia wakijeruhiwa katika mlipuko wa gesi Embakasi

February 2nd, 2024 1 min read

NA FATUMA BARIKI

WATU wawili wamethibitishwa kufariki, wengine 222 wakijeruhiwa huku mamia wakichomekewa na nyumba Alhamisi usiku kufuatia mlipuko wa gesi katika eneo la Mradi, Embakasi.

Kulingana na taarifa ya Msemaji wa Serikali, lori ambalo nambari zake za usajili bado hazijatambulika lililokuwa limebeba mitungi ya gesi lililipuka na kusababisha moto mkubwa kusambaa kwingi.

Mtungi mmoja wa gesi ulifyatuka na kugonga godown moja linaloshughulika na ushonaji nguo na kulichoma lote.

Moto huo pia ulichoma magari, nyumba za kibiashara pamoja na biashara nyingi.

Aidha, nyumba za makazi pia zilifikiwa na moto huo huku wakazi wengi wakikutwa wakiwa ndani ya nyumba zao.

Waliojeruhiwa wamekimbizwa katika hospitali mbalimbali huku serikali ikisema eneo la mkasa limedhibitiwa na polisi.