Kimataifa

Wawili wauawa kwenye makabiliano na polisi

September 14th, 2020 1 min read

Na AFP

Watu wawili wamefariki na wengine 14 kujehuriwa kwenye makabiliano ya risasi ambayo yalitokea Rochester, Newyork walisema polisi.

Maafisa waliotikia mwito wa kudumisha amani walijipata kwa kizaazaa huku watu zaidi ya 100 wakitoroka, kulinga na  mkuu wa polisi eneo hilo Mark Simmons.

“Kwa jumja tuna waathiriwa 16 wa makambiliano hayo. Nina huzuni kutangaza kwamba wawili kati ya ha 16 wamefarik,” alisema.

Waliofariki ni mwanamume na mwanamke wote wa miaka 18 na 22 lakini “hatukuwatambua majina yao.”

“Walioumia wamepelekwa hospitali huku wakiwa na majeraha madogo,” alisema.

Hakuna mtu aliyekamatwa kufikia sasa hivyo polisi hawawezi kusema kama ni mtu mmoja au wengi waliohusika kwenye makabiliano hayo.

Tafsiri na Faustine Ngila