Wazalendo hoi nchini Ghana

Wazalendo hoi nchini Ghana

Na GEOFFREY ANENE

TIMU ya pekee inayowakilisha Kenya kwenye mashindano ya mpira wa magongo ya klabu za Afrika, Wazalendo ilijikwaa katika mechi yake ya ufunguzi dhidi ya Zamalek nchini Ghana, jana.Vijana wa kocha Fidhelis Kimanzi walipoteza nafasi mbili nzuri wakilemewa na Wamisri hao 2-1 katika mechi ya Kundi B.

ugani Theodosia Okoh mjini Accra. Wazalendo, ambao watalimana na Ghana Revenue hapo Novemba 25, walijipata chini 1-0 katika dakika ya nane wakati Zamalek ilipata kona fupi na kutumia nafasi hiyo kikamilifu. Wakenya pia walipata kona fupi katika robo ya tatu, lakini haikuzalisha goli.

Wazalendo ilisawazisha 1-1 kupitia Wycliffe Mbeda mapema katika robo ya mwisho. Ilipoteza nafasi mbili ikiwemo kona fupi kabla ya kufungwa bao la pili na kuishia kudondosha alama zote.

Wazalendo, ambayo inarejea katika mashindano haya tangu 2007, itamaliza mechi za makundi dhidi ya Tairat kutoka Misri mnamo Novemba 27

You can share this post!

Wasimamizi wapya wa Ligi Kuu kuteuliwa leo

Simbas wahitimisha ziara na Wahispania

F M