Wazalendo: Tulipata mafunzo kwa kupigwa kwa hivyo hatukutoka mikono mitupu

Wazalendo: Tulipata mafunzo kwa kupigwa kwa hivyo hatukutoka mikono mitupu

Na AGNES MAKHANDIA

NAHODHA wa klabu ya mpira wa magongo ya wanaume ya Wazalendo, Job Omondi amekiri kuwa timu hiyo ina kazi kubwa ya kufanya kufika kiwango cha kuwania taji la Afrika.

Akizungumza baada ya Wazalendo kurejea nyumbani kutoka nchini Ghana ilikoshiriki mashindano ya Afrika jijini Accra, Omondi alisema kuwa mchezo huo umebadilika sana na wanahitaji kuenda na wakati. Wazalendo ilipoteza dhidi ya Zamalek 2-1, Ghana Revenue 1-0 na Tairat 4-2 katika mechi za Kundi B ugani Theodosia Ikoh.

Omondi alisema kuwa Kenya iko nyuma katika mchezo huo. “Ni wazi kuwa mapira wa magongo umebadilika sana na lazima tukubali mabadiliko…. Hata hivyo, kwa timu ambayo haikuwa imeshiriki ligi kwa miaka miwili kufunga mabao dhidi ya timu hizo kali, ni kitu cha kutia moyo,” alisema mshambuliaji huyo.

“Tulikuwa na wachezaji chipukizi ambao walijituma, na ingawa hatukuwa na bahati, tulipata mafunzo ya kututia moyo. Matumaini yetu ni kuwa tutakapofuzu tena, tutakuwa timu tofauti,” alisema. Wazalendo ilifuzu kushiriki mashindano hayo kwa kumaliza Ligi Kuu mwaka 2019 katika nafasi ya pili nyuma ya mabingwa Butali Sugar.

Butali hawakusafiri kwa sababu ya ukosefu wa fedha. Tairat ilitwaa taji kwa kupepeta Wamisri wenzao Zamalek 7-2 katika fainali.

You can share this post!

Mwanamke amwagia mpango wa kando Petroli

Wakufunzi zaidi ya 400 wameshtaki vyuo vikuu viwili kwa...

T L