Wazalendo yazuru Accra kushiriki mashindano ya hoki Klabu Bingwa Afrika

Wazalendo yazuru Accra kushiriki mashindano ya hoki Klabu Bingwa Afrika

Na TITUS MAERO

Timu ya midume ya Magongo ya Wazalendo iliondoka nchini jana alfajiri kushiriki kwenye mashindano ya Klabu Bingwa ya Afrika.

Kikosi hicho kilimaliza kampeni ya Ligi Kuu ya Hoki msimu uliopita katika nafasi ya pili, nyuma ya Mabingwa Butali Warriors ambao wamesusia kipute hicho cha haiba kubwa.Kivumbii hicho cha Afrika kinang’oa nanga mnamo jumatano Novemba 24 na kutamatika Novemba 30, 2021.

Timu hiyo ya Wazalendo inashirikisha wachezaji 18, maafisa 7 na mpuliza kipenga mmoja ambaye ni James Maina Chege. Hata hivyo, mkufunzi msaidizi wa timu hiyo Joseph Njogu aliteuliwa kuwa kocha mkuu wa timu hiyo.Njogu alichukuwa usukani kutoka kwa mkufunzi mkuu wa timu hiyo Fidelis Kimanzi ambaye kwa sasa anaandaa timu ya taifa ya Hoki ya Kenya.

Kocha Wycliffe Momanyi aliteuliwa kuwa mkufunzi msaidizi wa Wazalendo ambayo inatoka jijini Nairobi.?Jana, Katibu wa Klabu hiyo ya Wazalendo James Were alisema mabadiliko hayo ni ya muda mfupi.?’Kocha wetu mkuu Kimanzi ameagizwa na Chama cha Magongo nchini (KHU) kuanza matayarisho ya timu ya taifa,’ Were aliambia Taifa Leo kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta.

Were aliongeza kuwa kikosi chake kimefanya mazoezi ya hali ya juu na akaeleza kuwa watapambana na wapinzani wao kikamilfu.?’Niko na wachezaji wenye talanta pevu katika mchezo huo na wengine huchezea timu ya Hoki ya taifa la Kenya ,’ aliongeza.

Alitaja wachezaji hao kuwa madifenda John Rioba na Dennis Mwanzo.?Viungo wanashirikisha Griffin Okombe, Clifford Omari na Richard Njuki?Mafowadi wanajumuisha Danstan Barasa, Supciff Usagi, Mathew Momanyi na Joseph Kasua.

Mashindano ya mwaka huu ya Klabu Bingwa yamepangwa katika makunfi mawili.?Timu za kundi A zinajumuisha Eastern Company kutoka Egypt, Ghana Army, Ghana Police Service, Kada Stars (Nigeria) na Police Machine (Nigeria).

Kundi B linashirikisha Ghana Ghana Revenue Authority, Tairat (Egypt) Wazalendo (Kenya) na Zamalek E (Egypt).

You can share this post!

Onyo la Man City kwa wapinzani wao Uefa

Madai ya uzinzi yatishia kuvunja ndoa ya Kaparo

F M