Habari Mseto

Wazazi motoni kwa kumwadhibu mtoto hadi kifo

October 29th, 2020 1 min read

GEORGE ODIWUOR NA FAUSTINE NGILA

Polisi katika eneo la Ndhiwa wanachunguza kisa kimoja ambapo kijana wa miaka minne alifariki bada ya kuadhibiwa na wazazi wake kwa madai kwamba aliiba chakula jikoni.

Kijana huyo kwa jina Leon Bahati alifariki Jumapili Kijiji cha Ochol Kanyamwa Kusini kwenye mazingira yasiojulikana lakini wazazi wake waliambia polisi kwamba mwanao alifariki baada ya kunaguka kutoka mtini.

Wawili hao walidai kwamba mwanao alifariki baada ya kutereza na kunguka..

Ata hivyo wezake walisema kwamba kijana huyo alifariki baada ya kupokea kichapo cha ubwa kutoka kwa wazazi wake .

Watoto hao walimbia polisi kwamba mwendazaje alifariki baada ya kuathibiwa vibaya na wazazi wake kwa madai ya kuiba chakula jikoni.

Chifu wa Kanyamwa Kaskazini Daniel Opanda alisema kwamba kisa hicho kiliripotiwa kwa mzee wa Kijiji ambaye alienda kwenye eneo la tuko akiwa na polisi kutoka kituo cha polisi cha Ndhiwa.

“Wazazi hao tayari walikuwa washaanza matayarisho ya kumzika mwananwe kwani walikuwa na matatizo ya kifedha hawangemudu kupeleka mwili wa mwanao kwenye chumba cha kuhifadhi maiti,”alisema.

Lakini maafisa wa polisi walishuku walipoona majeraha kwenye mwili wa Bahati mapajani na mgogoni.