MALEZI KIDIJITALI: Wazazi wawe mfano mzuri wa vifaabebe!

MALEZI KIDIJITALI: Wazazi wawe mfano mzuri wa vifaabebe!

Na BENSON MATHEKA

ENZI hizi ambazo mawasiliano yamerahisishwa kwa sababu ya upatikanaji wa simu za mikono, wazazi wanafaa kuwa makini kupigana na habari zinazopotosha watoto wao kwa kuwa mstari wa mbele kutumia vyema vifaa hivi.

Wataalamu wa malezi dijitali wanasema kuwa wazazi wanafaa kuwa waangalifu wanapozungumza kwa simu wakiwa karibu na watoto wao kwa kuwa wanaiga tabia zao.

“Mtoto hata awe mchanga kiasi ngani, huwa anakua akiiga tabia za mzazi wake. Wazazi wanaweza kuanza kupalilia mbinu bora na salama za mawasiliano kwa watoto wao kwa kuhakikisha kuwa hawatumii lugha isiyo na heshima wanapowasiliana kwa simu wakiwa nyumbani au karibu nao. Kwa mfano, ikiwa umezoea kupayuka au kugombana kwa simu mtoto wako akisikiliza, ataiga tabia hiyo,” asema mtaalamu wa malezi Joyce Ibeka.

Ibeka anasema kuwa watoto wanaoiga tabia nzuri za wazazi wao, hukua wakiwa na tabia nzuri pia. Anasema kwa kuhakikisha watoto hawaigi matumizi mabaya ya teknolojia ikiwemo mawasiliano, wazazi wanajenga ustahimilivu kwa watoto wao.

“Sio wazazi pekee, walezi wanaoachiwa jukumu la kutunza watoto wanafaa kuwa na tabia nzuri wanapopotumia vifaabebe mbele ya watoto wao,” asema Ibeka.

Mtaalamu wa malezi dijitali Dkt Sameer Hinduja anaeleza kuwa wazazi wanastahili kuepuka matamshi ya chuki, uchochezi wakiwasiliana kwa simu au vifaabebe. Hii itafanya watoto kupalilia maadili mema, kuepuka matamshi ya kuudhi na hasira.

“Pia wanafaa kuwaeleza watoto athari za matamshi haya ili wakue wakifahamu kwamba hakuna mtu anayepaswa kudhulumiwa,” asema.

Mtaalamu huyu anasema kwa kufanya hivi, watawafunza watoto wao huruma, uvumilivu, heshima na utu wema kwa jumla.

“Funza watoto maana na matumizi ya vifaabebe ili kuwasaidia kujenga maisha yao na sio kuzua mitafaruku. Unaweza kufanya hivi kwa kuyatekeleza katika mawasiliano na matumizi yako mema,” asema.

You can share this post!

Mjue rafiki mnafiki

Lewandowski afunga mabao mawili na kusaidia Bayern...

T L