Wazee waidhinisha Waiguru awanie ugavana tena 2022

Wazee waidhinisha Waiguru awanie ugavana tena 2022

Na KNA

BARAZA la wazee kaunti ya Kirinyaga limemwidhinisha Gavana Ann Waiguru kutetea kiti chake likisema rekodi yake ya maendeleo inashinda ya wanaotaka kumpinga.

Baraza hilo limesema litawapiga msasa wagombea wote wanaosaka ugavana katika kaunti hiyo 2022.

Wazee hao walisema kwamba wanaomezea mate kiti cha ugavana katika kaunti hiyo ni sharti wawe wameonyesha rekodi ya maendeleo waliofanikisha na maono ya wazi kuhusu jinsi ya kuinua kaunti hiyo katika kiwango cha juu zaidi.

Akizungumza baada ya kukutana na Gavana Anne Waiguru nyumbani kwake, mwenyekiti wa baraza hilo Dkt Cyrus Githaka alisema kiti hicho kimevutia wagombea wengi hivyo basi kuna haja ya kumpata aliye bora zaidi miongoni mwao.

Bw Githaka alisema wanaowania wadhifa huo hawana chochote cha kuonyesha kuhusu maendeleo waliyofanikisha.

 

You can share this post!

FAUSTINE NGILA: Usilie ughali wa mafuta, nunua gari la...

Ghost Mulee kupigwa jeki na kuwasili kwa Olunga