Wazee wakemea viongozi kunyamazia mzozo wa bahari

Wazee wakemea viongozi kunyamazia mzozo wa bahari

Na MAUREEN ONGALA

WAZEE wa Kaya wanaotoka jamii ya Mijikenda na viongozi wa kidini wamewakashifu wanasiasa kutoka Pwani kutokana na kimya chao kuhusu mzozo wa mpaka kati ya Kenya na Somalia.

Wakuu hao wa kidini na wazee hao wamewataka wanasiasa hao wazinduke na kuwa mstari wa mbele kupigania sehemu ya nchi yao isitwaliwe na Somalia.Wiki jana, Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) iliamua kuwa sehemu ya Pwani mwa nchi ni ardhi ya Somalia ila wazee hao wanasema mahakama hiyo inafaa kuwapa ushahidi uliochangia uamuzi huo.

“Wanasiasa wetu wanafaa wazungumzie huu mzozo wa mpaka hapa na tena katika kiwango cha kitaifa na kimataifa. Kauli zao zitavutia hatua ichuliwe na serikali ili kuulinda mpaka wetu ndipo tusipoteze rasilimali zetu,’“Pia viongozi wetu wakiendelea kukashifu uamuzi wa ICC, hata Somalia itafahamu kuwa hili si suala la kufanyiwa mzaha,” akasema Askofu Amos Lewa Mwenyekiti wa muungano wa makasisi wa dhehebu mbalimbali Pwani.

Naye Mwenyekiti wa Muungano wa Wazee wa Kaya Mwinyi Mwalimu alisema uamuzi wa ICC ulikuwa na dosari na akamtaka Rais Uhuru Kenyatta ahakikishe kuwa anatekeleza wajibu wake wa kulinda mpaka wa Kenya kama amiri jeshi mkuu wa nchi.

“Alipoingia mamlakani baada ya uhuru, kulikuwa na mipaka ambayo iliwekwa na wakoloni na Somalia haikulalamika. Kwani waliibua kesi hii ilhali walikimya wakati marais wengine walikuwa mamlakani?’’ akauliza Mzee Mwalimu.

You can share this post!

Biden akemea Otrega kuwafunga wapinzani wake

Majaji watano wa mahakama ya juu waamuru Kananu aapishwe...

T L