Kimataifa

Waziri Mkuu Somalia ajiuzulu

July 26th, 2020 1 min read

ABDULKADIR KHALIF na FAUSTINE NGILA

Waziri Mkuu wa Somalia alijiuzulu Jumamosi baada ya wabunge kupitisha mswada wa kumtoa mamlakani.

Wabunge walipitisha mswada wakutokuwa na imani na waziri huyo jijini Mogandishu.

Wabunge hao walisema kwamba alifeli kwenye mipango yake kama kuchelewesha uchanguzi na kukosa kutekeleza programu za kudhamini kanuni za kikatiba.

Jumamosi jioni Bw Khaire alihutubia wanahabari huku akitaja kujiuzulu.

“Nimeamua kuwa mfano kwa watu wa Somali kwa kujiuzulu kutoka kwa nafasi niliyoshikilia watu wa Somali,”alisema Waziri huyo Khaire.