Habari Mseto

Waziri wa Viwanda ahusika kwenye ajali

October 26th, 2020 1 min read

NA FAUSTINE NGILA

Bodaboda moja iligongana na gari lililokuwa limebeba Waziri wa Viwanda Betty Maina Jumatano usiku.

Bi maina abaye hakuumia alikuwa amendeshwa na dereva wake nyumbani kkwa kutumia fgari la kazini wakati ajali hiyo ilipotokea kwenye barabara ya Kericho-Litein.

“Pikipiki moja iligogana na gari ya Waziri ya ofisini karibu na Jericho wakati Bi Maina alipokuwa akielekea nyumbani,”alisema Kamishena wa kaunti ya Kericho Karungu Kamau.

Bw Kamau alisema kwamba pikipiki hiyo iligoga gari hilo na nyuma saa tatu usiku.

“Haakuna mtu yeyeoye aliyeumia kwenye ajali hiyo na Waziri alikuwa salama,” aliongeza.

Bi Maina alikuwa kwenye ziara zake za kuchunguza miradi ya serikali maeneo ya Bonde La Ufa.