Waziri wa zamani Henry Rotich alilipa kampuni ya Italy SH8BN

Waziri wa zamani Henry Rotich alilipa kampuni ya Italy SH8BN

Na RICHARD MUNGUTI

KAMPUNI moja ya Italy iliyopewa kandarasi ya kujenga mabwawa ya Arror na Kimwarer imeishtaki Serikali ya Kenya ikiomba ilipwe zaidi ya Sh80bilioni kwa madai ilinyang’anywa kazi hiyo.

Ravenna Itinera Joint Venture imewasilisha kesi hiyo katika mahakama ya kutatua mizozo ya kimataifa mjini Hague nchini Uholanzi. Ravena imefichua aliyekuwa waziri wa hazina kuu ya kitaifa Henry Rotich aliinyang’a kazi hiyo na kuipa kampuni ghushi kwa jina Cmc Di Ravenna-Itinera Joint Venture.

Akitoa ushahidi wa utangulizi katika kesi ya ufisadi wa Sh63bilioni dhidi ya Bw Rotich, kiongozi wa mashtaka Taib Ali Taib alisema sheria haikufuatwa wakati wa kutoa kandarasi hiyo. Bw Taib alimweleza hakimu mkuu Lawrence Mugambi, kuwa kampuni hiyo ghushi ililipwa Sh8bilioni zilizokopwa benki za Italy.

Mahakama iliambiwa pesa hizo Sh8bilioni zililipwa kupitia benki za Ulaya.Mahakama ilifahamishwa Bw Rotich alikaidi sheria za utoaji zabuni na ulipaji pesa za umma. Mahakama ilijulishwa kampuni hiyo ghushi ililipwa pesa hizo ilikuwa haijasajiliwa.

You can share this post!

AKILIMALI: Jinsi bidhaa za sodo zinazoweza kudumu hadi...

Tim Wanyonyi Ngamia One FC, City Park zaanza vyema

T L