Habari Mseto

Wengi hawana ujuzi wa kazi licha ya kufuzu vyuoni – Ripoti

July 16th, 2019 1 min read

Na CECE SIAGO

VIJANA wengi katika kaunti za Pwani wanakosa kujiunga na vyuo vikuu baada ya kikamilisha masomo katika shule za upili.

Jumuia ya Kaunti za Pwani (JKP), kikundi kilichoundwa ili kuzingatia vipaumbele vya maendeleo pwani katika utafiti wake, imesema kwamba vijana wengi hawana ujuzi wa kazi na wengi hawajahitimu masomo katika vyuo vikuu

Mkurugenzi Mkuu wa kikundi hicho cha JKP Emmanuel Nzau alisema vijana hao hawana ujuzi wa kufanya kazi licha ya wengi wao kufuzu katika vyuo vikuu.

Alieleza kuwa kikundi hicho kinahusisha mashirika tofauti ili kuhakikisha kuwa vijana wamepata nafasi za ajira baada ya kusoma katika vyo vikuu.

“Miezi ambayo imepita tumekuwa tukifanya utafiti ili kujua sababu za vijana kukosa ajira na suluhisho zake. Matokeo ambayo tumepata ni kuwa wengi hawana ujuzi wowote. Kwa hivyo tunashirikiana na vyuo vikuu vilivyo katika mkoa huu wa Pwani,” Bw Nai alieleza.

Akiongea jana katika mkutano huko Mombasa ambao ulihudhuriwa na washirika wengine kutoka sekta mbalimbali za elimu alisema kuwa wanatarijia kuwa zaidi ya vijana elfu kumi watajiunga na vyuo vikuu mwaka huu.

Kampuni tofauti zimeahidi kuajiri vijana ambao watakuwa wamepata mafunzo ya ujuzi mbali mbali.