Wengi wanufaika na mafunzo kutoka kwa shirika la Engage Jamii Initiatives

Wengi wanufaika na mafunzo kutoka kwa shirika la Engage Jamii Initiatives

NA FARHIYA HUSSEIN

ZAIDI ya wakazi 200 kutoka eneo la Likoni kaunti ya Mombasa siku ya Jumatano walihamasihwa kuhusiana na suala la dhuluma za kijinsia na njia za kukwepa wabakaji.

Shirika la Engage Jamii Initiatives ndilo linaloendesha mpango huu unaolenga kaunti za Nairobi, Mombasa na Kajiado na ambao umedhaminiwa na Ubalozi wa Amerika nchini Kenya.

Walengwa watanufaika na mradi huu hadi Julai 2023.

“Tulionelea ni bora zaidi tukiwahamasisha kupitia wasanii na wanamuziki. Watu wengi mtaani siku hizi wanasikiliza muziki hivyo hii itakuwa njia rahisi kuwafikia walengwa,” alisema Mkurugenzi wa Shirika hilo Bi Fatuma Juma.

Aliongezea kuwa visa vya dhuluma za kijinsia vimekithiri eneo la Likoni ndiposa wakaja na mradi huo kupigana na visa hivyo.

“Idadi ya visa hivi iko juu katika hospitali ilhali katika vituo vya polisi ni kidogo. Hii ina maana bado haki zao hazijatimizwa,” alisema Bi Juma.

Alirai serikali na washika dau husika kuingilia kati na kujenga nyumba za usalama kwa waathiriwa na kuwaokoa kutokana na dhuluma wanazozipitia.

Wiki iliyopita shirika hilo iliweza kuhamisha watoto zaidi ya 250.

Watoto hao wa kati ya umri wa miaka 10 mpaka 17 walipokea mafunzo ya masuala kadhaa yakiwemo namna ya kupiga ripoti endapo watatendewa au kushuhudia dhuluma za kijinsia.

Mhubiri Bi Justine Kitaa alielezea umuhimu wa nyumba za maficho kujengwa huku akisema watoto wengi wanatoroka makwao na kuacha shule bila pahali pa kukimbilia wanapopata na na dhulma hizi za kijinsia ila ikiwa serikali itafanikiwa kujenga nyumba hizi basi itapunguza visa hivi.

Shirika hilo linanuia kuwafunza wanajamii na kutoa mafunzo wakiamini ni njia moja wapo ya kupunguza visa hivi vilivyokithiri katika eneo la Likoni.

  • Tags

You can share this post!

Yeye hugeuza uchafu kuwa sanaa inayolipa

Obiri na Korir kushindania ubingwa wa Ras Al Khaimah Half...

T L