Wenye vipande vya ardhi Diani waonywa kupoteza endapo wataendelea kutelekeza raslimali hiyo muhimu

Wenye vipande vya ardhi Diani waonywa kupoteza endapo wataendelea kutelekeza raslimali hiyo muhimu

NA SIAGO CECE

MABWANYENYE wanaomiliki ardhi kubwakubwa Diani, Kaunti ya Kwale, wameonywa watapokonywa ardhi hizo na serikali ikiwa hawatazitumia.

Wamiliki wa ardhi hizo ambao wengi wao hawaishi Kwale wamelaumiwa kwa kuacha ardhi yao wazi, na kuathiri mapato ya kaunti.

Gavana Fatuma Achani alisema ardhi hizo zikijengewa vivutio vya utalii au majengo ya kibiashara, itafaidi kaunti na pia kutoa nafasi za ajira.

“Pia tutaongeza kodi wanayolipa wenye mashamba hayo ili kufidia mapato ambayo kaunti ingepata ikiwa ardhi hiyo ingetumika,” Bi Achani akasema.

Wadau wa utalii walisema kutotumia ardhi hizo pia hufanya wahalifu wazitumie kama maficho na kuhangaisha wageni Diani.

  • Tags

You can share this post!

Wachukuzi walia SGR ikiwanyima biashara

Shirika lakusanya saini kupiga marufuku Kilimo cha...

T L