Wetang’ula sasa ataka Raila akamatwe

Wetang’ula sasa ataka Raila akamatwe

NA SHABAN MAKOKHA

WANDANI wa Naibu Rais Dkt William Ruto, sasa wanawataka maafisa wa usalama wamkamate kiongozi wa ODM Raila Odinga, baada ya kinara huyo wa upinzani kutumia neno ‘madoadoa’ akiwa katika ziara ya kampeni Wajir wiki jana.

Seneta wa Meru Mithika Linturi, alitumia neno hilo kwenye mkutano wa kampeni Uasin Gishu mnamo Januari 2, 2022, akakamatwa kabla ya kushtakiwa mahakamani.

Kiongozi wa Ford Kenya Bw Moses Wetang’ula, jana Jumapili alisema kuwa Bw Odinga anafaa kunyakwa na sheria itekelezwe jinsi ilivyokuwa kwa Bw Linturi.

Alisema hatua ya Tume ya Kitaifa ya Uwiano na Utangamano (NCIC), kumwagiza Bw Odinga afike mbele yake haitoshi na sheria inafaa kutekelezwa bila ubaguzi.

“Hakuna mtu ambaye yupo juu ya sheria. Ili kudhihirisha kuwa sheria inatekelezwa kwa usawa kwa Wakenya wote, tunataka kuona DCI na afisi ya DPP pamoja na ile ya NCIC zikichukua hatua na kuhakikisha kuwa kiongozi huyo wa ODM anakamatwa jinsi Bw Linturi alivyofanyiwa,” akasema Bw Wetang’ula.

  • Tags

You can share this post!

Aibu tupu mke wa mwanasiasa kukataa kuandalia wafuasi chai

Lenku apigwa jeki wazee wa Agikuyu wakiunga azma ya kutetea...

T L