Habari Mseto

Wezi wa M-Pesa wazimwa na umati

October 25th, 2020 1 min read

GEORGE ODIWUOR NA FAUSTINE NGILA

Washukiwa wawili walivamiwa na wananchi Jumatano kaunti ndogo ya Rachuonyo Mashariki baada ya kuvamia na kuiba dula la M-Pesa.

Washukiwa hao walivamiwa na wananchi walipokuwa wakijaribu kutoroka baada ya kuiba Sh 300,000 kwenye duka moja la Mpesa.

Mwenye duka hilo la Mpesa alikuwa ametoa pes ana alikuwa ananeleka kwa duka lake eneo la Miruka kwaa kutumia bodaboda wakati washukiwa hao walimvamia.

Mwenye duka hilo la Mpesa alisema kwamba wanaume wanne walisamisha bodaboda hilo alilokuwa akiendesha Kijiji cha Basi kwenye barabara ya Kisii-Miruka na kujitambulisha kuwa maafisa wa polisi..

Waliagiza ashuke kutoka kwa pikipiki hilo waingie kwa gari..

Kamanda wa polisi wa Rachuonyo Mashariki alisema kwamba washukiwa hao walikuwa wamejihami na bunduki.

Mwathiriwa huyo alisema kwamba majambazi hao walimfunga mikono kwanza kabla ya kumuibia.

“Washukiwa hao walikuwa wameejihami na Pistol.Walinisimamisha kabla ya kufika Miruka na kutoa Pistol na nikawasikiza ili kuokoa Maisha yangu,”alisema mwathiriwa huyo.