Wezi wa nyaya za stima bungeni taabani

Wezi wa nyaya za stima bungeni taabani

Na RICHARD MUNGUTI

WANAUME wawili walikiri walikamatwa na wafanyakazi wa kampuni ya Kenya Power wakiiba nyaya za kusambaza umeme katika majengo ya Bunge la Kitaifa na Majumba mengine makuu ya Serikali.

Francis Kuria Mwangi na Nicholas Mungai walikiri mbele ya hakimu mkazi Bi Sharon Maroro kuwa walivuruga nyaya za stima zinazosambaza umeme katika majengo kwenye barabara ya Uhuru Highway.

Nyaya walizokamatwa nazo zilikuwa za thamani ya Sh60,000.

Tayari washtakiwa walikuwa wamefaulu kukata mita 20 mnamo Julai 3, 2021.

“Washtakiwa walikutwa na Sururu , Koleo tatu na Msumeno wa kukata waya,” alisema kiongozi wa mashtaka.

Wezi hao wakamavu walishtakiwa kuiba nyaya za stima kinyume cha kifungu nambari 169 za sheria za Nishati.

Mwangi na Mungai walikuwa wameweka nyaya walizokuwa wamefaulu kukata kwenye gunia.

Wawili hao waliomba msamaha wakisema “ni shida tu inayowafanya kuiba.”

Mahakama iliamuru idara ya urekebishaji tabia wawahoji washtakiwa kabla ya kusomewa hukumu Julai 14, 2021.

You can share this post!

Sihitaji kuungwa mkono na Uhuru kuingia Ikulu – Raila

Bawabu aliyeingia kwa nyumba aliyolinda kusaka chakula...