Wezi wa parachichi wasakwa Kakuzi

Wezi wa parachichi wasakwa Kakuzi

Na RICHARD MUNGUTI

POLISI walilazimika kufyatua risasi mara tatu kuwashtua genge la majambazi saba waliokuwa wanaiba parachichi katika shamba la Kakuzi kaunti ya Murang’a.

Walipotakiwa kujisalamisha majambazi hao waliwarushia maafisa wa polisi parachichi hizo kabla ya kutorokea mle shambani.Hatimaye mmoja wa washukiwa hao alikamatwa akiwa na kilo 350 za parachichi.

Mshukiwa huyo alijaribu kuwahonga polisi na kitita cha Sh42, 300 katika kituo cha Polisi cha Kenol.Afisa mkuu wa polisi kituoni humo Martin Odwori alikataa kupokea mlungula huo na badala yake kuziweka fedha hizo kama ushahidi.

Malumbano makali kati ya polisi na wezi hao wa parachichi yalianza mwendo wa saa kumi unusu alfajiri maafisa kutoka kitengo cha kupambana na uhalifu DCI walipopashwa habari wizi ulikuwa unaendelea mle shambani la ekari 43,000 lililoko kwenye barabara ya Kenol-Sagana.

Maafisa hao walifika pale kuchunguza kilichokuwa kinaendelea.“Punde tu maafisa hao walipowasili waliona kundi la wanaume wakivuna parachichi aina ya Hass zinapelekwa masoko ya ng’ambo kuuzwa,” afisa msimamizi wa polisi eneo hilo alisema.

Wanaume hao walikuwa wanapakia parachichi hizo ndani ya gari aina ya Toyota iliyokuwa imeengeshwa kando ya barabara.Afisa mkuu wa polisi eneo hilo Bw Alexander Shikondi alithibitisha kisa hicho na kusema walifaulu kumtia nguvuni mshukiwa mmoja na gari lililokuwa linapakiwa parashishi hizo.

Washukiwa wenigine walitoroka.

  • Tags

You can share this post!

Pande zote zakubaliana kumsukuma Bashir ICC

Raila asema amepata mbinu kuteka Mlima