Habari Mseto

Wezi wa simu motoni

August 24th, 2020 1 min read

Na Richard Munguti

Washukiwa wawili wa wizi wa mabavu walikanusha kuwanyang’anya wananchi simu katika steji ya Makina, Kibra, Kaunti ya Nairobi.

Ramadhan Aziz Nassur na Zeid Oketch walikanusha mashtaka matatu ya wizi wa mabavu mnamo Agosti 5 mwaka huu.

Walikana walimnyang’anya Brian Otieno simu muundo wa Samsung yenye thamani ya Sh75,000.

Shtaka la pili dhidi yao ilikuwa ya kumnyang’anya Bervin Onyango simu muundo wa Hones yenye thamani ya Sh32000.

Pia walishtakiwa kwa wizi wa simu wa iPhone iliyo na thamani ya Sh32000.

Kwa jumla watatu hao walishrakiwa kwa wizi wa simu zilizo na thamani ya Sh139000.

Mahakama iliamuru idara ya urekebishaji tabia iwasilishe ripoti ya washtakiwa hao kabla ya kuachiliwa kwa dhamana.