Habari Mseto

Wezi wawili wanaswa wakiiba Lenana

July 2nd, 2020 1 min read

SARAH NANJALA na FAUSTINE NGILA

Maafisa wa kitengo cha upelelezi waliwakamata wezi wawili walionaswa na kamera za CCTV wakiibia mtu mmoja katika barabara ya Lenana Nairobi.

Walikamatwa wakiwa wamejificha maeneo ya Kawangware,Gatina na Pangani.

“Washukiwa wanne wa wizi walionaswa na kamera za CCTV katika Barabara ya Lenana Juni 25 wamekamatwa hii leo asubuhi na maafisa wa kitengo cha DCI wa Kilimani. Wanne hao walikamatwa wakiwa mafichoni Kawangware,Gatinana Pangani.”

Wawili hao Timothy Jahan Muzami  mwenye miaka 27 na Humphrey Minyata anayejulikana kwa jina la utani kama ‘Daddy’ mwenye miaka 23  alikamatwa kabla ya wiki kuisha baada ya video hiyo kuenea kwenye mitandao ya kijamii.

Katika video hiyo majambazi hao wanaonekana wakimtishia mwathiriwa kwa kisu na bunduki baada ya kumuibia simu na mfuko wake mchana peupe.

Muzami anaonekana akimpiga mwathiriwa huyo ambaye hajulikani kichwani kwa kutumia bunduki kabla ya kumuibia mfuko huku Minyata akiwa ameigiza mikono yake kwenye mifuko ya mwathiriwa ya nguo akitafuta simu.

Maafisa hao pia walikamata Mary Wambui 23 na Ali Musa 26 wanaoaminika kuwa walikuwa kati ya kikundi hicho cha majambazi.

Bi Wambui anaaminika kuwa alikuwa amemficha jambazi mmoja kwa nyumba yake Pangani.

Mkurungezi wa kuchunguza maswala ya uhalifu George Kinoti alisema kwamba wanne hao wako kizuizini wakigonja kufikishwa kortini.