WhatsApp kuanza kutekeleza masharti mapya Jumamosi

WhatsApp kuanza kutekeleza masharti mapya Jumamosi

Na SAMMY WAWERU

MTANDAO  wa kijamii wa WhatsApp sasa umetoa tangazo la kuongeza masharti zaidi ili kuboresha mtandao wake.

Sheria na mikakati hiyo inatarajiwa kuanza kutekelezwa Jumamosi ya Mei 15, 2021.

Aidha, tangazo hilo limetolewa na kujitokeza mara kwa mara kwenye skrini mtumizi anapoingia kwenye mtandao wa WhatsApp.

“Fahamisho la sheria na mikakati ya WhatsApp…Kwenye tangazo hili, tunaongeza maelezo kwenye sheria na mikakati yetu, inayojumuisha unavyoweza kuwasiliana kupitia jumbe za biashara, ukichagua.

“Nayo ni pamoja na; Biashara zinavyoweza kudhibiti jumbe zake, maelezo zaidi kuhusu WhatsApp inavyofanya kazi – tunavyounda data na kuhakikisha akaunti yako ni salama. Mifano ya tunavyofanya kazi na Facebook ili kutoa bidhaa mpya na huduma,” linaeleza tangazo hilo, ilani hiyo pia ikiarifu sheria na mikakati hiyo itaanza kutekelezwa Mei 15, 2021.

“Tafadhali, itikia fahamisho hili ili uendelee kutumia mtandao wa WhatsApp makataa yatakapokamilika,” inasema ilani.

Mtandao huo hata hivyo umehakikishia watumizi jumbe zao zitakuwa salama licha ya mabadiliko hayo.

“Hatuwezi tukasoma wala kuskiza jumbe zako za kibinafsi, kwa sababu ni kati yako na unayezungumza au kujadiliana naye. Sheria hiyo haitabadilika,” apu hiyo inaelezea.

You can share this post!

Kilifi Ladies FC yaomba kushiriki ligi ya Pwani

Jubilee haitambembeleza Kuria, atatimuliwa chamani –...