‘Wiki ya Lugha za Kiafrika’ ni mwamko mpya kuhusu nafasi ya lugha za kiasili katika elimu

‘Wiki ya Lugha za Kiafrika’ ni mwamko mpya kuhusu nafasi ya lugha za kiasili katika elimu

NA BITUGI MATUNDURA

MBONA tunaonea aibu lugha zetu za asili? Jibu la swali hili linapatikana katika kuitalii hali ya jinsi ambavyo wakoloni walivyozichukulia lugha zetu.

Wakoloni waliotawala Afrika ni pamoja na Wafaransa, Wajerumani na Waingereza.

Mataifa yaliyotawaliwa na Wafaransa na Waingereza bado yana mihuri ya lugha za watawala wao. Mataifa mengi ya Afrika Magharibi hutumia Kifaransa kama lugha yao rasmi (Benin, Ivory Coast, Guinea na Togo n.k). Nigeria, Ghana, Sierra Leone na Gambia hutumia Kiingereza kuwa lugha yao rasmi.

Hali hii pia inaonekana Afrika Mashariki na Kati na kusini mwa Afrika. Wafaransa walisisitiza ukuzaji wa Kifaransa katika shule za maeneo waliyotawala. Hii leo, chambacho mtaalamu Pierre Alexandre, wasomi wengi katika maeneo hayo wanajua Kifaransa kupindukia na wamezama katika utamaduni wa Wafaransa kuliko wanavyojua lugha na utamaduni wao.

Hata hivyo, hali ilikuwa tofauti katika himaya za Waingereza. Waingereza angalau walijihusisha na ukuzaji wa lugha za Kiafrika. Wasomi wengi Waingereza walijifunza lugha na tamaduni za Waafrika na kuchapisha vitabu vingi vya lugha hizo – zikiwemo kamusi na vitabu vya sarufi. Wataalammu hao ni pamoja na R.C. Abraham, A.H. Kirkgreene, John Spencerg miongoni mwa wengine.

Huku wageni wakizama katika utafiti kuhusu lugha za wenyeji wao, Waafrika walizidharau lugha zao na kuziona kuwa ‘shenzi’ na za hadhi ya chini.

Maadhimisho ya Wiki ya Lugha za Kiafrika (Januari 24 -30) yanaibua mwamko mpya na kuhusu nafasi ya lugha hizo katika mifumo ya elimu.

  • Tags

You can share this post!

MWALIMU WA WIKI: Martin Gitonga

Dhana ya Utamaushi inavyokuzwa katika ‘Chozi la Heri’

T L