Wimbo waelezea hisia za Uhuru akiachana na Ruto

Wimbo waelezea hisia za Uhuru akiachana na Ruto

NA STEPHEN MUNYIRI

WIMBO maarufu wa mapenzi kutoka kwa jamii ya Agikuyu “Reke Tumamwo” (wacha tuachane), ulichukua mkondo wa siasa katika mkutano wa “Sagana 3”, Rais Uhuru Kenyatta alipomshambulia naibu wake akisema hafai kuongoza nchi.

Wimbo huo wa miaka ya tisini ulioimbwa na msanii Peter Kigia, ulitumika kuvuta pumzi kila rais aliporusha kombora zito kwa “nduguye” William Ruto, huku hadhira ya wafuasi wa chama cha Jubilee ikicheza wimbo huo na kumshangilia.

Tungo hilo, ‘Reke Tumanwo’, lililpobuka kuwa maarufu sana katika mkutano uliofanyika kwenye hoteli ya Sagana, ni hadithi ya marafiki wa zamani, ambao waliamua kutengana kila mmoja akiamua kubeba mizigo yake.

Hisia za Rais Kenyatta alipokuwa akihutubu, zilijitokeza kwenye wimbo huo ambao maneno yake yaliashiria ujumbe wenye hasira. Mhusika mkuu anachoshwa na mpenzi wake ambaye amebadilika na kuwa mbwa mwitu aliyevalia mavazi ya kondoo.

Kwenye wimbo huo, anamweleza mwenzake kuwa siku imewadia wao kuachana.

“Leo nimeamua tuachane, hata kama tuna uhusiano, wacha kila mmoja aende njia yake. Iwapo kuna mmoja wetu aliyekuwa kimelea kwa mwenzake, wacha sote tubebe mizigo. Muda wa kuwa mizigo umekwisha,” unaeleza ubeti wa kwanza wa wimbo huo.

Rais alimshutumu naibu wake kuwa mfisadi asiyeaminika huku akiwaomba Wakenya, wasimwamini wala kumpea nafasi ya kuongoza nchi. Kama wimbo huo unaositisha urafiki wa muda mrefu, Rais Kenyatta alitia kikomo kwa ndoa yao ya kisiasa iliyosheheni misukosuko.

Rais alikuwa akihutubia maelfu ya wakazi kutoka eneo la Mlima Kenya ambapo alielezea sababu za kumtema Dkt Ruto na kumkumbatia kinara wa ODM, Raila Odinga.

Kwenye kikao hicho, mjini Sagana, alimpa Raila baraka kumrithi Agosti.

  • Tags

You can share this post!

Ruto kuzuru USA, Uingereza siku 12

Fainali ya UEFA msimu huu yahamishwa kutoka Urusi hadi...

T L