Habari Mseto

Wiper, CCM zaingia Jubilee

June 17th, 2020 1 min read

NA DAVID MWERE

Kinara wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka ametia sahihi mkataba wa ushirikiano kati ya chama chake cha Wiper na chama tawala cha Jubilee.

Katika mkutano uiliowekwa kwenye afisi za chama cha Jubilee Pangani, Nairobi Bw Kalonzo alikuwa ameandamana na Seneta wa Makueni Mutula Kilonzo Junior, Chirau Mwakwere na Judith Sijeny.

Katibu wa chama cha Jubilee Raphael Tuju na Naibu Katibu David Murathe walikuepo.

Katika mkutano huo kinara wa Chama Cha Mashinani Isaac Ruto pia alitia sahihi mkataba na chama cha Jubilee, katika mchakato unaotajwa kama mpango wa Jubilee kuvimeza vyama vidogo.

Bw Musyoka na Ruto wanaonekana kutamanishwa na azma ya Rais Kenyatta kuwashirikisha wanasiasa anaoamini watamsaidia kutekeleza miradi yake kabla ya kung’atuka hapo 2022.