Wito kwa vinara wa NASA waungane upya

Wito kwa vinara wa NASA waungane upya

Na JUSTUS OCHIENG

KUNDI la viongozi katika Muungano wa National Super Alliance (Nasa) wanataka kukomeshwa kwa malumbano miongoni mwa vinara wao, kuhusu anayepasa kugombea urais 2022.

Walisema vinara hao wanne wa Nasa – Raila Odinga (ODM), Kalonzo Musyoka (Wiper), Musalia Mudavadi (Amani National Congress) na Moses Wetang’ula wa Ford Kenya, ni sharti waandae kikao ili kusuluhisha tofauti zao.

Manaibu wenyekiti wa Wiper Mutula Kilonzo Jnr, na Victor Swanya pamoja na Katibu Mkuu wa Ford Kenya, Bw Chris Wamalwa, walisema hawafutilii mbali uwezekano wa viongozi hao kufanya kazi pamoja tena.

“Wanapofanya hivyo, wanampiga jeki Naibu Rais bila kujua. Raila kama kiongozi wa muungano ni sharti akumbuke haifai kutawanya kila mtu. Itakuwa pigo kwake si ushindi,”

Bw Kilonzo alieleza Taifa Leo.

You can share this post!

Kifo cha Mbunge chaongeza mkosi kwa Bunge la 12

Mwilu alalamikia rundo la kesi kortini