Habari Mseto

Wito kwa wazazi mitaani wapeleke wana kwa taasisi za ufundi

April 18th, 2019 1 min read

NA SAMMY KIMATU

WAZAZI wameombwa kuwapeleka wana wao kwenye taasisi na vituo vya kufunza ufundi badala ya kutegemea elimu ya kawaida.

Aidha walishauriwa kupalilia vipaji vya wanao na kuwaonyesha maadili mema wakati wanatangamana na jamii ili nidhamu kwao iwe ni nzuri.

Hayo yalinenwa Alhamisi na msimamizi wa kanisa la katoliki la St Monicah mtaa wa mabanda wa Mukuru-Lunga Lunga, Kaunti ya Nairobi, Bw Samuel Osoro.

Aliongea wakati wa kufuzu kwa mahafala 148 katika kituo cha Mukuru Skills Training Centre (MUST) kilichoko mtaani humo alipokuwa mgeni wa heshima.

“Maadili yamepotea miongoni mwa wanafunzi wetu tangu kiboko kiwekwee chini ndiposa vijana wanauna na mizozo ya urafiki kukithiri,” akasema Bw Osoro.

Jumla ya wanafunzi 148 walifuzu kwa taaluma mbalimbali zikiwemo ushonaji nguo, urembo, ufundi na ualimu wa shule za chekechea pamoja na upishi.

Mshirikishi wa hafla hiyo Bi Anne Muthoni kutoka Mukuru Slums Development Project anmabo husimamia kituo hicho alihimiza wazazi pia kuelekeza watoto kuchukua kozi mbalimbali na kujiepusha na kasumba ya kutilia maani kusopma kwa kawaida bila taaluma nyingine.

“Ni bora kuwa na taaluma yako akilini kuliko kitu unachoshika mkononi kwa vile hauwezi ukapokonywa,” Bi Muthoni akasema.

Katika hafla hiyo, wanafunzi waliwatumbuiza wageni kwa nyimbo, acrobati, mashairi na mchezo wa kuingiza.