Ngirici ataka wahudumu wa bodaboda kujiepusha na uhalifu

Ngirici ataka wahudumu wa bodaboda kujiepusha na uhalifu

Na KNA

MBUNGE Mwakilishi wa Kirinyaga Wangui Ngirici amewataka wahudumu wa bodaboda katika eneo kujiepusha na vitendo vya uhalifu.

Bi Ngirici pia aliwashauri waendeshaji bodaboda hao kuwa waangalifu na kuchunguza wale wanaofanya biashara nao wasije wakawahudumia wateja watakaotumbukiza katika shida.

Alisema imebainika kuwa baadhi ya wahalifu wanawatumia wahudumu wa bodaboda kuendesha uhalifu.

Bi Ngirici alisema hayo Jumamosi katika mkahwa wa Sifa Gardens mjini Kutus alipozindua rasmi Chama cha Akiba na Mikopo cha wanabodaboda mjini humo kwa jina Kutus Riders Operators Sacco.

“Nimewahakikishia kuwa nitawasaidia ili mjiimarishe. Lakini nangependa kuwaomba mjiupushe na vitendo vya uhalifu. Pia mjihadhari ili msije mkutatumika kufanikisha shughuli za uhalifu,” akaeleza.

Bi Ngirici alielezea imani kuwa atachaguliwa kuwa Gavana wa Kirinyaga katika uchaguzi mkuu wa 2022.

“Nikichaguliwa gavana mwaka ujao nina imani kuwa nitakuwa nikipatikana kwa urahisi kwa sababu nimezaliwa, kulelewa na kuolewa hapa Kirinyaga. Kwa hivyo, siwezi kuwatelekeza watu wetu,” akasema Bi Ngirici.

Tafsiri: CHARLES WASONGA

You can share this post!

UDA yaanza kuyumba

Weta aamua ni Lusaka tosha ugavana 2022

T L