Wizara kufunza wakazi kilimo cha kibiashara

Wizara kufunza wakazi kilimo cha kibiashara

Na WINNIE ATIENO

WIZARA ya Kilimo imewaahidi wakulima katika Kaunti ya Kwale kwamba watapewa mafunzo ya kilimobiashara ili waweze kuzalisha mazao bora zaidi.

Katibu Mkuu wa Kilimo Prof Hamadi Boga alisema makundi matatu ya kila wadi katika kaunti hiyo watapewa mafunzo.

“Alafu tutawapatia vifaa vya nyuki kwa wale wanaofuga nyuki, mbegu za pojo, kunde, tomato, sukuma wiki ili waweze kuzalisha mazao bora. Watapewa mafunzo katika taasisi ya kilimo cha Karlo na mashirika mengine ili wapate ujuzi wakutosha,” alisema Prof Boga.

Prof Boga ambaye aliandaa maonyesho ya Kilimo huko Kwale aliahidi kuwezesha wakulima ili wajimudu.

“Tutageuza hali zetu kupitia kilimo biashara. Tuna bahati kuwa na mashamba ambayo yanaweza kuzalisha vyakula,” aliongeza Prof Boga ambaye amejitosa katika siasa za Kwale akiwania ugavana.

You can share this post!

Wizi wa taa, alama za trafiki vyanzo vya ajali – KeNHA

DPP aamuru Mkenya apelekwe Amerika kushtakiwa

T L