Kimataifa

Wanafunzi 100 wapatikana na corona Zimbabwe

November 17th, 2020 1 min read

AFP NA FAUSTINE NGILA

Wanafunzi mia moja wa shule ya upili nchini Zimbabwe wamepatikana na virusi vya corona, serikali ilisema Jumanne huku hbari hiyo ikizua hofu kwamba kuna maaambukizi mapya ya virusi hivyo.

“Wanafunzi mia moja wamepatikana na virusi vya corona  kwenye shule ya upili ya John Tallach Matabeleland Kaskazini,”msemaji wa serikali Nick Magwana alisema kwenyee ujumbe wa Twitter.

Hakusema ni lini vipimo hivyo vilichukuliwa lakini alisema kwamba shule hiyo inawanafunzi Zaidi ya 600,shule yenyewe imefungwa hakuna mtu yeyote anaruhusiwa kuingia ndani”.

Kwa sasa Zimbabwe imerekodi visa 8,897 vya corona huku nchi jirani ya Afrika Kusini ikiwa na visa 750,000 na  vifo 20,314.

Shule zilifungwa mwezi Machi baada ya kuzuka kwa virusi vya corona huku zikifunguliwa Septemba wakati virusi vya corona vilianza kupungua.