Habari Mseto

Yaibuka kampuni inayotaka kununua Unga Group ilikiuka sheria

February 21st, 2018 1 min read

Na BERNARDINE MUTANU

KAMPUNI ya Marekani inayopanga kununua sehemu ya Unga Group inachunguzwa kwa kukiuka sheria za kifedha.

Kampuni hiyo Seaboard Corporation inasemekana kukiuka sheria hizo nchini Kenya na mataifa mengine ya Afrika.

Kampuni hiyo inachunguza na serikali ya Marekani kwa visa vingi vya uhalifu ikiwemo ni pamoja na ufisadi, utoaji wa hongo, kuosha fedha na kufanya biashara na zilizoorodheshwa na serikali kwa kutenda makosa.

Hata hivyo, kampuni hiyo inasemekana kushirikiana vyema na wachunguzi na imejitayarisha kupata uamuzi wa aina yoyote, unaoipendelea, au usioipendelea.

Mwaka wa 2014 na 2016, kampuni hiyo pia ilichunguzwa kuhusiana na kuosha fedha katika operesheni zake.