Habari Mseto

Yaibuka wizara zilishindwa kupangia Sh200 bilioni

August 22nd, 2018 1 min read

Na BERNARDINE MUTANU

WIZARA na mashirika ya serikali zilishindwa kutumia zaidi ya Sh200 bilioni katika mwaka wa kifedha wa 2017/2018.

Hii ni kulingana na Wizara ya Fedha katika ripoti iliyowasilisha Bungeni. Hali hiyo imetia katika mizani uwezo wa serikali kutimiza ahadi zake.

Kulingana na ripoti hiyo, hiyo ilionyesha uwezo hafifu wa wizara za serikali kutekeleza miradi chini yake.

Kulingana na Wizara ya Fedha, kiwango cha fedha kilichotumika katika miradi iliyofadhiliwa na mashirika ya kimataifa pia kilikuwa cha chini sana.

Wizara na mashirika hayo zilishindwa kutumia Sh218.5 bilioni. Hivyo serikali kwa jumla ilitumia Sh2.11 trilioni, badala ya kiwango kilicholengwa cha Sh2.33 trilioni.