Habari Mseto

Yassin Juma kuishi Ethiopia

August 28th, 2020 1 min read

NA FAUSTINE NGILA

Mwanahabari wa Kenya aliyezuiliwa nchini Ethiopia sasa yuko huru kurudi nyumbani, lakini ameamua kushini jijini Addis Ababa na marafiki zake.

Bw Yassin Juma, ambaye alipata virusi vya corona, aliruhusiwa kutoka kwenye eneo ya kujitenga baada ya kumaliza siku 14 za kujitenga.

Ubalozi wa Kenya Ethiopia alisema kwamba Bw Juma, ambye jina lake kamili ni Collins Juma Osemo alikuwa huru kurudiĀ  nyumbani baada ya kuachiliwa kutoka kituo cha polisi na kituo cha afya cha Woreda ambapo alikuwa ametengwa.

“Aliachiliwa Jumatano Agosti 26 2020. Wakati aliachiliwa alikuwa keshamaliza siku za kujitenga 14 ujumbe kutoka maswala ya nchi za kigeni ulisema.”