Habari Mseto

Yaya aliyejitetea bosi alimpa Sh800,000 baada ya uroda atupwa ndani

December 1st, 2019 1 min read

Na Joseph Ndunda

Mwanamke aliyedai kuwa bosi wake alimwekelea Sh800,000 kifuani baada ya kumburudisha kimapenzi, Ijumaa alifungwa jela miaka mitatu kwa wizi.

Ruth Khaecha alipatikana na hatia ya kuiba Sh1.3 milioni mali ya mwajiri wake Paul Kanyi Mwangi ambaye alidai alimwekelea kifuani kama zawadi baada ya kufanya mapenzi naye.

Alipokuwa akijitetea, Khaecha alisema aliamua kumpagawisha Kanyi aliyemuita katika chumba chake cha kulala amsaidie kupanga bahasha alizokuwa nazo lakini wakachangamkiana kimapenzi.

Alisema katika hali hiyo, Kanyi alimueleza kwamba bahasha hizo zilikuwa na pesa na binafsi alithibitisha ilikuwa kweli.Alisema baada ya kufanya mapenzi, Kanyi aliwekelea bahasha moja kwenye maziwa yake.

Lakini kwenye uamuzi wake Hakimu Mkuu wa Makadara Heston Nyaga alipuuza madai hayo akisema hayakuweza kuthibitishwa.

Alisema Khaecha aliambia walinzi kwamba alikuwa ametumwa kupeleka nguo kwa fundi zikashonwe walipomuuliza alichokuwa akibeba alipoondoka kwa mwajiri wake.