Habari Mseto

Yaya anayedaiwa kuiba Sh1m aachiliwa kwa dhamana ya Sh700,000

June 28th, 2019 1 min read

Na RICHARD MUNGUTI

YAYA mwenye umri wa miaka 30 ameshtakiwa kwa kumnyang’anya kimabavu mwajiri wake Sh1 milioni.

Emma Njeri Wangeci alikanusha mashtaka mawili mbele ya hakimu mkazi Bi Martha Nanzusi.

Alidaiwa mnamo Feburuari 28, 2019 katika eneo la Westlands, Nairobi akishirikiana na watu wengine na kumnyang’anya kimabavu mwajiri wake Bi Neena Manhlarlar Shah Sh1,140,000na dhahabu, simu ya kiunga mbali na kipakatalishi.

Shtaka la pili ni la kupatikana na mali ya wizi.

Alishtakiwa kuwa alienda katika benki ya Equity na kukamatwa akiweka Sh750,000 katika akaunti yake akijua hela zimeibwa au kupatikana kwa njia isiyo halali.

Mahakama ilimwachilia kwa dhamana ya Sh700,000 pesa taslimu