Yaya ashtakiwa kwa kuojesha mvulana wa bosi wake “Sukari”

Yaya ashtakiwa kwa kuojesha mvulana wa bosi wake “Sukari”

Na RICHARD MUNGUTI

MJAKAZI aliyekuwa na mazoea ya kumwojesha mvulana wa mwajiri wake “sukari” yake alishtakiwa jana kwa kumnajisi mtoto huyo.

Bi Sabina Mwikali Muasya mwenye umri wa miaka 22 alikabiliwa na mashtaka mawili ya kunajisi na kuwadhulumu kimapenzi watoto wawili wa mwajiri wake mwaka uliopita.Sabina alikana aliwadhulumu kimapenzi watoto wa mwajiri wake kwa muda wa miezi sita alipokuwa akiwalea mtaani Kileleshwa kaunti ya Nairobi.

Hakimu mkazi mahakama ya Milimani Bi Jane Kamau alifahamishwa na kiongozi wa mashtaka kwamba Sabina alimnajisi mvulana wa miaka 12 kwa kushiriki ngono naye.Mbali na shtaka hilo la kumnajisi mvulana huyo, Sabina alikana alikuwa anaiguza sehemu nyeti ya mvulana huyo mwenye miaka 12.

Hakimu na umma uliokuwa mahakamani walishtushwa na madokezo ya kiongozi kwamba mshtakiwa “alikuwa anamlazimisha dada yake mvulana huyo mwenye umri wa miaka mitano kunyonya sehemu nyeti za nduguye.”Mahakama ilifahamishwa kisa hicho kilifichuliwa na dada yake mvulana huyo mjakazi mpya alipoajiriwa.

Msichana huyo mwenye umri wa miaka mitano alimwuliza mjakazi wao mpya ikiwa atakuwa anamlazimisha kuoja kwa mdomo wake sehemu nyeti ya nduguye jinsi Sabina alikuwa “anawasimamia kutenda aibu.”Mjakazi huyo mgeni hakunyamazia habari hizo.

Alimjulisha mama ya watoto hao.Uhalifu huo uliripotiwa katika kitengo cha polisi cha kushughulikia dhuluma dhidi ya watoto na wanawake.Mshtakiwa alishtakiwa alitekeleza uhalifu huo kati ya Januari na Julai 2020 katika mtaa wa Kileleshwa.

Polisi walimsaka mshtakiwa na kumpata nyumbani kwao kaunti ndogo ya Matuu kisha wakamkamata.Sabina aliomba mahakama imwachilie kwa dhamana.“Naomba hii mahakama iniachilie kwa dhamana isiyo ya kiwango kikubwa. Niko na mtoto mdogo aliye na umri wa miezi mitatu.

Anahitaji kutunzwa sana nyakati hizi za maradhi ya Corona,” Sabina alimsihi hakimu.Upande wa mashtaka haukupinga mshtakiwa akiachiliwa kwa dhamana ila aliomba korti iamuru idara ya urekebishaji tabia imhoji mshtakiwa na watu wao kabla ya kuachiliwa kwa dhamana.

Bi Kamau aliamuru mshtakiwa azuiliwe katika gereza la Lang’ata hadi Septemba 1,2021 ripoti ya urekebishaji tabia itakapowasilishwa kisha uamuzi wa dhamana utolewe.

  • Tags

You can share this post!

Viongozi wa kutoka Mlima Kenya wakutana Thika kuweka...

Mfanyabiashara akiri kuiba Sh0.2m kupitia Mpesa