Yaya asukumwa jela miaka 5 kwa kumlisha mtoto kamasi

Yaya asukumwa jela miaka 5 kwa kumlisha mtoto kamasi

NA RICHARD MUNGUTI

YAYA aliyemlisha mtoto wa umri wa miezi mitano kamasi na kumlambisha ute wa sehemu zake nyeti amefungwa jela miaka mitano.

Catherine Mukoya Nalianya, 20, alisukumwa gerezani na hakimu mkazi mahakama ya Milimani Nairobi Bw Festus Terer anayesikiliza na kuamua kesi za watoto.

“Hii mahakama imekupata na hatia ya kumtendea mtoto mchanga dhuluma mbaya kwa kumlisha kamasi kutoka kwa pua yako. Pia ulikuwa unamlambisha ute uliochota kwa kidole kutoka sehemu zako nyeti,” Bw Terer alimweleza mjakazi huyo alipomhukumu.

Bw Terer alisema kitendo hicho hakiambatani na maadili mema ya ubinadamu na alimfanyia mtoto huyo unyama.

“Kitendo ulichomtendea mtoto huyo sio cha kibinadamu. Ni kitendo cha kiushetani na uhayawani,” hakimu alimweleza mshtakiwa.

Mahakama ilielezwa unyama huo uliguduliwa na mama yake mtoto alipotazama picha zilizonaswa na kamera za CCTV alizoweka ndani ya makazi yake katika mtaa wa Fedha ulioko Embakasi jijini Nairobi.

Akijitetea, mshtakiwa alieleza hakimu yuko na mtoto wa umri wa miaka mitatu na ndiye anayemshughulika ili kumkimu kimaisha.

Akipitisha hukumu, Bw Terer alisema mshtakiwa hastahili kuonewa huruma ikitiliwa maanani alimtendea unyama mtoto mchanga bila kujali iwapo atamuambukiza magonjwa au la.

Alisema mshtakiwa ni mama na pia amejaliwa kuzaa.

Catherine alipatikana na hatia ya kutenda uhalifu huo Julai 28, 2022.

Alipewa siku 14 kukata rufaa.

  • Tags

You can share this post!

Shirika lakusanya saini kupiga marufuku Kilimo cha...

Waluke ajisalimisha kwa polisi kupelekwa jela

T L