Zaidi ya Sh1.5M zachangiwa Congo Boys FC

Zaidi ya Sh1.5M zachangiwa Congo Boys FC

Na ABDULRAHMAN SHERIFF

ZAIDI ya Sh1.5 milioni zilichangwa kwa ajili ya mradi wa kununua basi la klabu ya Congo Boys FC katika tafrija iliyotayarishwa na Kamati ya Uwanja wa Serani Sports mjini Mombasa wakati wa tafrija maalum iliyofanyika usiku wa Ijumaa.

Katika tafrija hiyo ambayo pia ilitumiwa kuwatuza watu waliofanya vizuri katika Nyanja mbalimbali ikiwemo wenye kuhusika na michezo, klabu hiyo ya Congo Boys inakayoshiriki kwenye Ligi ya Kitaifa Daraja ya Pili, ilikuwa tayari imechangisha Sh1.5m kabla ya siku hiyo.

Harambee hiyo iliyoongozwa na Mbunge wa Mvita, Abdullswamad Nassir ambaye ana nia ya kupigania wadhifa wa ugavana, ilichangisha zaidi ya Sh1.5m zikiwemo zake Sh300,000, Jaffer Foundation Sh500,000 na Nassir akimchukulia dhamana Gavana Hassan Joho ya Sh500,000.

Wengine waliochagia ni anayetaka kuwania ubunge eneo la Nyali Said Abdalla almaarufu Saidoo Sh200,000 na anayepania kupigania ubunge eneo la Mvita Mohamed Machele Sh100,000 na mgombea mwingine wa kiti hicho Tawfiq Balala 100,000 kati ya wengine kadhaa.

Imebakia Sh1.3m kukamilisha bei ya kununulia hilo basi.Wanasiasa wengine waliokuwako na kutoa michango yao ni pamoja na Hassan Rajab Sumba Sh20,000, Mohamed Ali Juma Sh50,000, Diwani wadi ya Majengo Ahmed Khamis Nyundo na nduguye Salim Nyundo wakatia Sh50,000.

Mwenyekiti wa Serani Sports Ground (SSG) Alamin Mohamed ambaye pia ni kinara wa Congo Boys FC amesema ana matumaini makubwa wahisani watajitokeza kuhakikisha wanakamilisha pesa zinazohitajika Sh1.3m ili klabu hiyo ipate kufanikiwa kwa lengo lake la kuwa n abasi lao.

You can share this post!

Gavana ataka uchaguzi uahirishwe

Suala la ardhi latumiwa kama chombo kumega kura za Pwani

T L